MFUKO WA UINJILISHAJI
Mchango wako ni mbegu ya neno la Mungu. Tusaidie kufikia jamii za Wamasai, kulea vijana, na kueneza upendo wa Kristo kila kona ya Arusha.
Uinjilishaji ni kwa kila Mbatizwa; Kuinjilisha ni kufikisha Neno kwa maeneo husika yenye uhitaji pasipo kujali kabila wala rangi. Hivyo wote tunawajibika kuifanya kazi ya Uinjilishaji.
Kujenga na kuendeleza misioni mpya, vigango, parokia, pamoja na ununuzi wa ardhi kwa ajili ya upanuzi wa Kanisa katika maeneo yenye uhitaji.
Kusaidia gharama za usafiri na kutoa mafunzo kwa Mapadri, Watawa, na Makatekista ili waweze kulifikisha Neno la Mungu vijijini na pembezoni.
Kusambaza Biblia Takatifu, Misale, Katekisimu, na visakramenti; ikiwemo pia kununua vyombo vya usafiri (Magari, Pikipiki) kurahisisha huduma za kichungaji.
Kuandaa vipindi vya kidini kwenye Redio, TV, na mitandao ya kijamii, pamoja na kugharamia semina na makongamano ya kiinjilishaji kwa umati mkubwa.
Kusaidia uendeshaji wa vigango, na parokia changa pamoja na kuwekeza katika miradi inayoleta tija katika kuliimarisha Kanisa kijamii na kiuchumi.
Kupitia michango yenu, Mfuko umefanikiwa kufadhili miradi 14 kwa asilimia 60% yenye thamani ya TZS Milioni 224.3. Hapa kuna baadhi ya miradi hiyo mikubwa:
Tumewezesha ununuzi wa pikipiki na matengenezo ya magari kwa parokia za pembezoni ikiwemo Matui, Ngorongoro, na Mto wa Mbu ili kurahisisha uinjilishaji.
Ujenzi wa Kanisa Kigango cha Samunge (Mt. Yuda Tadei), Parokia ya Hippo, na ujenzi wa nyumba za mapadri Mbuguni na Simanjiro Kaskazini.
Kusaidia uendeshaji wa vipindi na miundombinu ya AMANI Radio FM kwa ufadhili wa TZS Milioni 59.4 ili injili iwafikie wengi zaidi popote walipo.
Tazama pikipiki mpya kwa ajili ya wamishenari vijijini
Kusaidia uinjilishaji vijijini.
Kufikia kila muumini.
Matunda ya michango yenu.
Huduma ya maji safi na salama kwa jamii zetu
Hatua za ujenzi zinazoendelea kutokana na michango ya waumini
Ndani ya Kanisa
Imekamilika Asilimia 100
Ujenzi Unaendelea
Mradi uliokamilika kikamilifu
Mapadri wakitoa huduma za kiroho katika jamii za wafugaji na vijijini
Engaruka, Arusha
Kila mchango wako unaofanya kupitia mtandao wa simu unatuwezesha kufikia asilimia kubwa ya lengo hili. Chagua kiwango chako leo na uwe Balozi wa Uinjilishaji!
Inasaidia kutoa kijitabu kimoja cha mafunzo ya dini kwa kijana mmoja mkoani.
Changia HapaInasaidia safari ya misheni ya siku moja kwa makatekista vijijini kwa ajili ya ubatizo.
Changia HapaInachangia uendeshaji wa promosheni ya kimtandano kwaajili ya mfuko, kama youtube adds, sms bulk push.
Changia HapaBuruta kielekezi chini kuona jinsi mchango wako unavyosaidia misheni yetu kijamii.
Inagharimia mafuta ya gari la safari ya misheni ya dharura vijijini.
MKOMBOZI BANK
01211520778901
Jina: CATHOLIC ARCHDIOCESE OF ARUSHA - UINJILISHAJI
TUMIA NAMBA: 58 KWA WALE WASIO MAPAROKIANI NA WENYE MAPENZI MEMA.
Ushuhuda kutoka kwa wale wanaoguswa na kazi yako ya uinjilishaji.
"Mfuko huu umesaidia sana kufikisha neno la Mungu katika maeneo ambayo awali yalikuwa magumu kufikika. Tunaona mabadiliko makubwa ya kiroho kwa watu wetu."
Padre Francis
Misheni ya Engaruka
"Kama kijana, nimepata nafasi ya kukua kiroho kupitia mafunzo na semina zilizofadhiliwa na Mfuko wa Uinjilishaji. Tunamshukuru Mungu kwa kila anayechangia."
Maria Lowassa
Umoja wa Vijana
"Mafunzo niliyopata yamenisaidia kuwa katekista bora. Sasa naweza kuwafundisha watoto na watu wazima neno la Mungu kwa ufasaha zaidi."
Yohane Mollel
Makatekista Arusha
Kila mchango wako unaambatana na baraka. Mbali na kusaidia ujenzi na maendeleo ya kiroho, tunapenda kuungana nawe katika sala. Tuma nia yako maalum ya sala hapa chini, na mapadri wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha wataziweka nia hizi katika Ibada ya Misa Takatifu.
Nia zako zinasomwa na kuwekewa ibada maalum katika makao makuu yetu ya Jimbo.
Unaweza kuchagua kutaja jina lako au kutuma nia yako kama siri (Anon). Mungu anaijua mioyo yote.
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa."
— Mathayo 7:7
Una swali au unataka kujua zaidi kuhusu kazi yetu? Tuandikie ujumbe hapa.
Ofisi Yetu
Arusha, Tanzania
Tupigie
+255 652 391 121
Asante sana kwa kutoa mchango wako. Taarifa zako zimepokelewa kwa ajili ya kuandaliwa stakabadhi. Mungu akubariki kwa ukarimu wako!